Full-Width Version (true/false)


Walimu wa alama kupewa kipaumbele katika ajira mpya za walimu.
Serikali imesema katika ajira mpya za walimu zitakatoka siku chache zijazo walimu wa alama ni moja kati ya makundi ambayo yamepewa kipaumbele kwenye ajira hizo. 

Naibu Waziri osi ya Rais-TAMISEMI Mhe.Josephat Kandege amesema hayo Bungeni mkoani Dodoma na kuongeza kuwa Serikali inatambua kuwepo kwa upungufu wa walimu wa elimu maalum. 

Aidha Naibu Waziri Kandege amewaagiza wakurugenzi wote wa halmashauri nchini kuhakikisha walimu waliosomea elimu maalum wanapelekwa katika shule hizo na siyo vinginevyo. 

Naibu Waziri Kandege alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa viti maalum Soa Mwakagenda aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kuajiri walimu wa alama hapa nchini

No comments

Powered by Blogger.