Full-Width Version (true/false)


Walimu wanaojitolea Zanzibar watakiwa kuomba Ajira Utumishi

 

Serikali  ya Mapinduzi ya Zanzibar imewataka walimu wanaojitolea katika Skuli mbalimbali za Serikali Unguja na Pemba kuomba nafasi  za ajira katika tume ya Utumishi  Zanzibar.

Akijibu hoja zilizoulizwa na wajumbe wa Baraza la wawakilishi wakati walipokuwa  wakichangia  hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar juu ya uwepo wa walimu wanajitolea  Waziri wa Wizara hiyo Riziki Pembe Juma amesema serikali inafahamu kuwa wapo walimu zaidi ya mia tano wanaojitolea na kuwataka walimu wenye sifa kuomba nafasi ili waweze kuajiriwa.

Nae Mwakilishi wa Jimbo la Chaani Nadir Abdul-latif amesema  walimu hao wamekuwa  na jitihada za kuomba nafasi za kazi kila zinapotangazwa na Tume ya Utumishi lakini wanakosa licha ya kuwa na sifa za kuajiriwa.

Wakati huo huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ amesema Sheria ya Utumishi wa Umma inazingatia  pia  mazingira ya maeneo kama wapo walimu  wenye sifa za kuajiriwa serikali  hutoa  kipaumbele.

Kwaupande wake Mwakilishi wa Viti Maalum  Nafasi za wanawake Zainab Abdalla ameiyomba serikali   kuboresha Elimu mjumuisho  ili walengwa waweze kunufaika na elimu hiyo ikiwemo kuajiriwa walimu wenye sifa pamoja na upatikanaji wa vifaa vinavyotakiwa.

No comments

Powered by Blogger.