Full-Width Version (true/false)


WALIOINDOA YANGA LIGI YA MABINGWA AFRIKA WATWAA UBINGWA BOTSWANA


Timu ya Township Rollers imefanikiwa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Botswana ikiwa ina pointi 66 kileleni na kufikisha taji la 15 la ligi hiyo.
Rollers walipoteza mchezo wa jana dhidi ya Security System kwa bao 1-0 lakini matokeo hayo hayajaweza kuwaathiri kwa chochote kutokana na pointi walizofikisha kutoweza kufikiwa na timu nyingine
Wapinzani wao Jwaneng Galaxy wamemaliza ligi wakiwa nafasi ya pili wakifanikiwa kujikusanyia alama 62 ambazo zinaipa nafasi ya Umakamu Bingwa.
Rollers wametwaa taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo na kuandika rekodi yao mpya tangu kuanzishwa kwa ligi hiyo.
Timu hiyo inakumbukwa kufuatia kuiondoa Yanga kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi wa mabao 2-1 na kuidondoshea kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika inayoshiriki hivi sasa.
25 May 2018

No comments

Powered by Blogger.