Full-Width Version (true/false)


Wanafunzi hukosa masomo zaidi ya miezi mitano kila mwaka.


 

Wanafunzi zaidi ya 120 katika kitongoji cha N'gese Lutali,kata ya Matuli wilayani Morogoro wamekuwa wakishindwa kwenda shule kwa zaidi ya miezi mitano kila mwaka kutokana na kushindwa kuvuka mto Ngerengere ambao hufurika maji nyakati za mvua.

Baadhi ya wazazi na viongozi wa kitongoji cha Ng'ese Lutali,kijiji cha Kwaba wilayani Morogoro wamesema wanafunzi wanaotoka kijijini hapo kwenda shule  ya kata jirani ya Selegete iliyopo kata nyingine ya Kidugalo ni magumu hasa wakati wa mvua  licha ya ya changamoto nyingine ya  wanafunzi kutembea zaidi ya saa moja na nusu kuka shuleni,na hata eneo wanakopita hakuna daraja. 

Wamebainisha wanafunzi kushindwa kwenda shule ya msingi Kwaba katika kata ya Matuli kutokana na umbali kuwa ni zaidi ya saa mbili ikilinganishwa na kata jirani, huku miundo mbinu ikiwa sio raki hivyo wakalazimika kumuomba mmoja wa watu  walioanza uwekezaji kwenye sekta ya kilimo katika kitongoji hicho, Stephen Nyakile, aliyewajengea darasa,osi,stoo na vyoo huku wao wakichanga tofali  na kutafuta msaada zaidi halmashauri ya wilaya kuendeleza ujenzi huo. 

Diwani wa kata ya Matuli Lucas Limomo amekiri kitongoji hicho kuwa na idadi kubwa ya wananchi ikilinganishwa na vitongoji vingine vya kata hiyo ambapo takwimu za wanafunzi 120 ni za uandikishaji wa mwaka 2015,na kushukuru kwa msaada wa ujenzi wa darasa uliotolewa.

No comments

Powered by Blogger.