Full-Width Version (true/false)


Wanafunzi wa kike waaswa kujithamini

Wanafunzi wa kike wameaswa kutokuwa bidhaa rahisi kwa kuepuka kurubunika na kujiingiza katika mapenzi hali inayoweza kuwasababisha kupata maradhi na mimba kabla ya wakati.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Ndola Masunga ametoa rai hiyo wakati akikabidhi jengo la maabara kwa Shule ya Sekondari Bulekela lenye thamani ya Sh. milioni 17.13.
Masunga aliwataka wanafunzi kujikita zaidi katika masomo kwa kutumia vizuri maabara hiyo katika masomo ya sayansi kwa vitendo ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao.
Alisisitiza kuwa ili waweze kufanikiwa wanahitaji kuepuka vishawisishi kutoka kjwa wananume ambao mwisho wa siku wanawakimbia na kuwaachia maradhi na mimba kabla ya wakati.
“Watoto someni kwa bidii haya maisha yapo tu msidanyike na wanaume ambaoi wakiwapa mimba wanawakimbia. Na nyie wavulana msidanyike eti mnaacha shule halafu ili muoe hilo halipo huwezi kuoa wakati huna shughuli ya kufanya, shule inakluongezea maarifa ya maisha,” alisisitiza.
Kwa upande mwingine Masunga ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii aliipongeza Bodi ya Shule na uongozi wake kwa kusimamia vizuri fedha na hatimaye kukamilika kwa mradi huo.
Aidha aliwataka walimu na wanafunzi kushikamana ili kuleta ufanisi katikma taaluma na hatimaye kutoa matokeo mazuri huku akiwataka wazazi kuwasimamia vizuri watoto wao na kuhudhuria shuleni bila kukosa.
Akiwasilisha taarifa ya mradi huo, Mkuu wa Shule ya Sekondari Bulekela, Mwalimu C. Chikoti alisema kuwa kazi zote zimefanyika kama ambavyo zilielekezwa kwa kiwango kilichohitajika.
Mwalimu Chikoti aliongeza kuwa fedha zilizokuwa zimebaki zilitumika katika shughuli ya upakaji wa rangi majengo mengine ya shule hiyo na kufanya mfanano katika muonekano wake.
Alitaja shughuli zilizofanyika ni pamoja na kuweka masinki ya zege katika vyumba vitatu, kunganisha mfumo wa maji safi, kujenga ngazi kwa kuzingatia mahitaji ya mbalimbali hasa walemavu na kupaki rangi nguzo za maabara.
Shughuli nyingine ni kuweka marumaru, kuziba mifereji iliyo inayopitisha maji, kuunganisha mabomba yote kwenye masinki kwa ajili ya kutoa maji taka nje ya maabara pamoja na kuweka dari mpya.    
Ujenzi wa jengo hilo la maabara umefadhiliwa na Serikali kupitia Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) huku wananchi wakichangia nguvu kazi katika kuufanikisha.


No comments

Powered by Blogger.