Full-Width Version (true/false)


Wanawake wa Rwanda na Kenya wataishi muda mrefuWanawake nchini Rwanda na Kenya ndio wanaotarajiwa kuishi muda mrefu zaidi miongoni mwa wanawake na wanaume katika nchi za Afrika Mashariki, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Shirika la Afya duniani (WHO). 
Umri wa wanawake kuishi Rwanda kwa sasa ni miaka 69.3 na nchini Kenya ni miaka 69.0.
Hata hivyo, umri wa kuishi wa wanaume Uganda ndio ulioongezeka zaidi katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita, ambapo umepanda kwa miaka 13.5.

Nchini Tanzania, umri wa kawaida wa kuishi kwa wanawake kufikia mwaka 2016 ulikuwa miaka 66, ongezeko la miaka 10 ukilinganisha na mwaka 1990 kwa mujibu wa Utafiti wa Mzigo wa Maradhi Duniani mwaka 2016, ulioratibiwa na Taasisi ya Takwimu za Afya na Utathmini.

Kwa wanaume, umri wa kuishi ulikuwa miaka 62.6 kufikia mwaka 2016 ukilinganisha na miaka 53.7 mwaka 1990. Kwa kiwango cha kadiri, umri wa kuishi kwa Watanzania umeongezeka kwa miaka kumi kufikia sasa tangu mwaka 1990.

Nchini Kenya, umri wa kuishi kwa wanawake umeongezeka kutoka miaka 62.6 mwaka 1990 hadi miaka 69 mwaka 2016, ongezeko la takriban miaka sita, lakini kwa wanaume ongezeko limekuwa ni kutoka miaka 60.2 hadi miaka 64.7, miaka 4.5.

Nchini Uganda, umri wa kuishi kwa wanawake sasa ni miaka 64.7 (sawa na umri wa wanaume kuishi Kenya) na kwa wanaume ni miaka 59.8.

No comments

Powered by Blogger.