Full-Width Version (true/false)


Wanawake waandamana kwa hasiraWanawake Nchini Kenya wameandamana leo mjini Nairobi kulalamika tuhuma za kufukuzwa kwa mwanamke mmoja katika mgahawa mmoja kwa kumyonyesha mtoto wake. 
Wanawake hao wameelekea katika mgahawa wa Olive Restaurant, ambako mama huyo anatuhumu kuwa aliambiwa ajifunike wakati anamnyonyesha mtoto wake mwenye mri wa mwaka mmoja.

Taarifa hiyo imezusha hisia za watu wengi nchini humo na kusababisha makundi ya kutetea haki za wanawake kuandaa maandamano.

Wakina mama hao wamesema maandamano ya leo ni kushinikiza haki za akina mama waungwe mkono na kusaidiwa katika kufanikisha kuwanyonyesha watoto wao bila ya ubaguzi wa aina yoyote.

No comments

Powered by Blogger.