Full-Width Version (true/false)


Wastara amtaja mbaya wake


Msanii wa muziki wa filamu bongo Wastara Juma amemtaja mtu ambaye yeye amemuita mbaya wake, anayemchafua kwenye mitandao ya kijamii kwa kumtuhumu masuala ambayo hayana ukweli. 
Wastara amesema anajua mtu anayeleta habari za uongo dhidi yake ni Mtanzania anayeishi nchini Marekani Mange Kimambi, na kusema kwamba huenda yeye ana uhakika kuwa hatapata matatizo kama binadamu wengine.

“Hii yote tangu ilipotokea upinzani, mimi nasema mpinzani wangu mkubwa alikuwa Mange, na yeye ndiye ambaye alikuwa anacomnt vibaya na wale waliokuwa wanasuport kwenye acount yake, nadhani hawa hawajahi kupitia matatizo, na siku wakifa watapaa mbinguni, familia zao zikiugua hawata pata matatizo, ndio maana wanakuwa hawana huruma”, amesema Wastara.

Wastara ameendelea kwa kusema kwamba anashangazwa na kitendo cha mwanamke huyo kumuonyesha chuki ilhali hajawahi kumkosea kitu, na kuwataka Watzania kuwa na huruma kwani lichaya kuwa yeye ni binadamu pia ni mama ambaye anahitaji kulea watoto wake.

No comments

Powered by Blogger.