Full-Width Version (true/false)


Watoto watoa mwili wa aliyekufa maji MtwaraWatoto wawili wenye umri wa miaka 8-12, wameibuka mashujaa baada ya kuokoa mwili wa mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Mzee Nampwenge aliyekufa na maji, baada ya kuzama kwenye bwawa alipokuwa akiogelea huko Namayanga, Naliendelea mkoani Mtwara. 
Akizungumza na mwandishi wetu mwenyekiti wa mtaa wa Namayanga Ally Salum Nayove amesema ni kweli watoto hao waliotambulika kwa majina ya Faraji Muhibu, na Islam Shaibu, wanaosoma darasa la nne na mwingine la pili ndio walioweza kujitosa kwenye bwawa hilo ambalo limejaa maji kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha, na kuutoa mwili huo.

Naye mzee Hamisi Nahoda  ambaye ni rafiki wa karibu wa Mzee Nampwenge aliyekuwa naye siku ya tukio wakiogelea, amesema kwamba rafiki yake huyo alikuwa anajikumbusha kuogelea lakini maji yalimzidi na kufariki dunia saa chache kabla ya kufuturu.

Kutokana na tukio hilo mwenyekiti Ally Salum Nayove  amewataka wananchi na watoto wadogo kutocheza katika maeneo hayo, ambayo awali yalikuwa ni machombo ya mchanga na sasa kujaa maji kutokana na mvua.
Mtoto Faraji Muhibu

No comments

Powered by Blogger.