Full-Width Version (true/false)


Watu 100 wafariki dunia kwenye ajali ya ndegeWatu zaidi ya 100 wamedaiwa kufariki dunia katika ajali ya ndege aina ya Boeing 737 iliyoanguka mjini Havana, Cuba Ijumaa hii.
Ndege hiyo ambayo ilikuwa ibebeba abiria 104 pamoja na wahudumu 6 ilianguka na kulipuka karibu na uwanja mkuu wa ndege wa Jose Marti. Imeelezwa kuwa Wahudumu wote sita wa ndege hiyo walikuwa ni raia wa nchini Mexico lakini abiria waliokuwa wamepanda ndege hiyo ni raia wa Cuba.Hata hivyo kwa mujibu wa mtando wa The Sun umesema kuwa, wanawake waliokolewa kutoka kwenye mabaki ya ndege hiyo wakiwa hai lakini hali zao ni maututi.
Serikali ya Cuba imeanzisha uchunguzi wa ajali hiyo na kutangaza siku mbili za maombolezo ya kitaifa. Ndege hiyo ilikuwa inatoka mjini Havana kwenda Holguin, Mashariki mwa Cuba.

No comments

Powered by Blogger.