Full-Width Version (true/false)


Watu 38 wafariki dunia baada ya kingo za bwawa kupasukaWatu 38 mpaka wameripotiwa kupoteza maisha huku zaidi ya familia 450 zikiyakimbia makazi yake mjini Nakuru nchini Kenya kufuatia kingo za bwawa la Patel lililopo katika eneo la Subukia kupasuka usiku wa kuamkia leo.Kufuatia tukio hilo tayari watu 47 wamekimbizwa katika hospitali ya Nakuru/Bahati huku jitihada za uokoaji zikiendelea mjini katika eneo hilo.


Shughuli za uokoaji zikiendelea

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mjini Nakuru, Japhet Kioko amesema kuwa jitihada za kutafuta miili mingine zinaendelea kwa kutoa matope yaliyoingia kwenye makazi ya watu.


Tayari Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ameshatoa salamu za rambi rambi kwa familia zilizopoteza ndugu, marafiki na jamaa kwenye tukio hilo. Soma taarifa yake iliyotolewa na Ikulu

No comments

Powered by Blogger.