Full-Width Version (true/false)


Watu walio na virusi vya Ebola Congo wameongezeka

Idadi ya watu waliothibitishwa kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola Jamhuri ya Demokrasi ya Congo imeongezeka hadi kufikia 14 Wizara ya afya imetangaza kesi nyingine 11 ambazo zimethibitishwa na kesi moja mpya inayohusiana na ugonjwa huo kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa siku ya Alhamisi kutoka wizara hiyo ilisema kuwa kesi zingine 11 mpya na kifo cha mtu mmoja zimeripotiwa katika mji wa Bikoro katika mkoa wa Equateur, mahali ambapo ugonjwa huo wa Ebola ulitangazwa kutokea May 8.

No comments

Powered by Blogger.