Watumishi wa Ofisi ya RC Arusha wabadilishiwa mashtaka Mahakamani

Ofisa Itifaki wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha, Swalehe Mwidadi na mfanyakazi wa Masijala Amina Mshana leo May 23, 2018 wamepanda kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha na kusomewa shtaka la unyang’anyi wa kutumia silaha.
Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa serikali Sabina Silayo mbele ya Hakimu Mkazi Patricia Kisinda, amedai kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja wanashtakiwa kwa makosa mawili.
Amedai kuwa kosa la kwanza, wametenda mnamo May 13, 2018
eneo la Sakina washtakiwa hao walimwibia Mwandishi wa Habari wa
kujitegemea Lucas Myovela simu aina ya Tekno C7 ya thamani ya
Sh.300,000, simu aina ya Sumsung yenye thamani ya Sh.50,000 na
walifanya unyang”anyi huo kwa kutumia panga na mkanda wa plastiki.
Aliendelea kutaja kuwa vitu vingine
walivyoiba ni pamoja na fedha taslimu Sh.75,000 na walijihamishia fedha
Sh.9,500 za Mpesa na kadi ya ATM ya benki ya CRDB, huku wakijuwa kufanya
hivyo ni kosa kisheria.
Silayo alidai kuwa kosa la pili was
wanashtakiwa kuwa mnamo May 13, 2018, eneo la Sakina kwa pamoja
walifanya kitenfo cha ukatili na udhalilishaji kwa kumvua Lucas Myovela
nguo zake na kumchukua picha akiwa uchi.
Alidai kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria na kufunguliwa kesi hiyo namba 153/2018.
Washtakiwa walikana mashtaka hayo na
Wakili Silayo amedai upelelezi haujakamilika na kuomba mahakama kupanga
tarehe nyingine ya kutajwa.
Hakimu Kisinda amedai kesi hiyo haina dhamana na shtaka la kwanza halina dhamana hivyo alipanga kutajwa tena June 5 mwaka huu.
No comments