Full-Width Version (true/false)


Wayne Rooney kutimkia DC United FC ya nchini Marekani



Mshambuliaji wa klabu ya Everton, Wayne Rooney anatarajiwa kujiunga na timu ya DC United inayoshiriki ligi kuu nchini Marekani kwa dau la pauni milioni 12 mara baada ya mchezo wake wa mwisho siku ya Jumapili.

Klabu kadhaa kutoka Major League Soccer (MLS) zimekuwa zikimfatilia, Rooney kupitia kwa wakala wake, Paul Stretford kwa zaidi ya mwaka mmoja kabla ya kurejea Goodison Park.

Habari zachini zinaaminika kuwa dili hilo limekamilika toka miezi miwili iliyopita baina ya wakala Stretford na Mkurugenzi Mkuu wa klabu ya DC United, Jason Levein.

Makubaliano hayo ambayo bado hayajasainiwa yatafikia tamati mwishoni mwa msimu wa mwaka 2020, lakini yakitegemea kwa kiasi kikubwa makubaliano baina ya Rooney na Familia yake.

No comments

Powered by Blogger.