Full-Width Version (true/false)


Waziri aingilia suala la upimaji DNA
Naibu waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile amesema kuwa si kila mtu ana mamlaka ya kuiagiza Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kupima vinasaba (DNA) na kwamba elimu inapaswa kutolewa ili kujua nani anapaswa kufanya nini wakati gani na kwa sababu gani. 
Dk. Ndugulile ameyasema hayo leo mapema alipokuwa akizindua Bodi tendaji ya kwanza ya maabara ya mkemia mkuu wa Serikal ambapo ameitaka bodi hiyo kusimamia na kuhakikisha elimu inatolewa kwa wananchi ili waelewe namna sahihi ya utendaji wake.

Amefafanua kwamba miaka ya hivi karibuni vinasaba vimekuwa vinaongelewa zaidi lakini jamii haitambui, taratibu na namna wanavyoweza kufuata taratibu na kupimwa.

Amesisitiza kuwa elimu ianze kutolewa kwa jamii kuelewa mwenye mamlaka ya kuviomba hivyo vipimo na kuielekeza maabara ya mkemia mkuu kuvipima.

"Tusije kufungua mambo ambayo hayapo, si kila mtu ana mamlaka ya kuiamrisha maabara ya mkemia mkuu kupima na kutoa majibu, kuna taratibu zake. Haya mambo ni ya kisheria, ukikosea kuchukua vipimo, kuagiza vipimo kesi hata kama ipo mahakamani inafutwa" Amesema.
Ameongeza "Siyo kila mtu anaweza kuiamrisha maabara ya mkemia mkuu kufanya vipimo vya vinasaba.

No comments

Powered by Blogger.