Waziri Mwakyembe asikitishwa na tukio la bondia kulipishwa hela na promota kwa huduma ya choo kwenye ndege
Moja kati ya vitu ambavyo vinausumbua mchezo wa ngumi nchini Tanzania
ni figisu fisuri za mapromota wa ngumi pamoja na viongozi wa mchezo
huo.
Hivi karibuni kuna tukio moja lisilo la kawaida limeripotiwa kutokea
ambalo inadai kuna promota mmoja aliweza kumtoza pesa bondia kwaajili ya
huduma ya choo ndani ya ndege.
Hayo amebainishwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo,
Dk. Harrison Mwakyembe akiwa kwenye kikao maalum ya wadau wa ngumi
nchini.
“Ngumi zetu zilipofikia ni aibu, hivi kweli promota unampeleka bondia
kupigana nje halafu unamtoza chakula cha kwenye ndege? Na huduma ya
choo? Huu ni uonevu mkubwa,”
Aliongeza, “Mabondia wengine wanapigwa ngumi za vichwani hadi
wanapata matatizo, lakini bado mnawadhulumu, nimeshaambiwa hili na
taarifa zake zote ninazo. Kuanzia sasa mikataba ya mabondia wanaokwenda
kupigana nje sharti iwe wazi.”
Pia, hakuishia hapo amewaonya pia vigogo wa vyama vya ngumi nchini;
Rais wa Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO), Yassin
Abdallah ‘Ustadhi’ na Rais wa PST, Emmanuel Mlundwa, kuwa wajitathimini
kwa tuhuma zinazowakabili za kuvuruga ngumi za kulipwa nchini.
No comments