Waziri Mwigulu Nchemba aishangaa Yanga
Mdau wa Singida Unite ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya ndani
ya Nchi Mwigulu Nchemba amesema anafurahishwa na mwenendo wa ligi kuu
Tanzania bara ambayo imefikia hatua timu ndogo inaweza kuifunga timu
kubwa.
Mwigulu amesema tatizo linaloisumbua kigi yetu kwa sasa ni kushindwa
kuwa na ushirikiano katika mashindano ya kimataifa jambo ambalo limekuwa
likitufanya kuwa mbali katika mashindano ya kimataifa kiasi cha
kushindwa na nchi kama Zambia.
Katika hatua nyingine kiongozi huyo amelilaumu shirikisho la soka
Tanzania TFF kwa kushindwa kutoa support kwa Yanga ambayo inasbiriki
michuano ya kkmataifa.
“Nikiona timu ndogo zinaanza kucheza kwa kuajiamini kama hivi unaona
Kagera Sugar inaweza kushinda uwanja wa taifa tena kwenye mechi ambayo
ina sherehe, ukiona Ihefu inakaribia kuitoa Yanga, Green Warriors inatoa
bingwa mtetezi naona kuna kujiamini flani kunaanza kujengwa kwa
wachezaji.”
“Zamani ilikuwa timu kubwa zikipangwa na ndogo, timu kubwa inapata matokeo kabla ya mechi lakini sikuhizi mambo yanabadilika.”
“Jambo ambalo bado ni tatizo ni mwendelezo wa ubora wa mchezaji
kwamba akiwa bora leo tumuone bora kesho na kuendelea iondoke ile
kuoanda na kushuka, sasa wachezaji wetu unaweza ukamuona bora sana leo
baada ya siku kadhaa akishasifiwa kidogo anajisahau.”
“Wakati mwingine hata timu nzima zinakosa mwendelezo wa ubora kwa
mfano Mbao iliyoifunga Yanga ukiiangalia kwenye mchezo unaofuata utaona
tofauti kubwa sana, timu nzima imepoteza ubora.”
“Vipaji vipo, wachezaji wanaanza kujiamini lakini shida ni kujisahau.
Kuna wachezaji bado hawajajua kama mpira ni biashara nzuri watu
wanajali mechi za ushabiki kwa mfano nilikuwa naongea na rafiki zangu wa
Yanga hivi karibuni baada ya kupoteza mechi dhidi ya Simba na matumaini
ya ubingwa kupungua, wakawa wanasononeka sana wanasema tujipange kwa
ajili ya msimu ujao.”
“Wanatafuta ubingwa ili wacheze mechi za kimataifa, lakini mechi za
kimataifa bado wanazo lakini hawaongelei hizo wanaongelea kujipanga kwa
ajili ya msimu ujao washindane na Simba. Hizo fikra nazo bado shida.”
“Badala ya kufikiria nafasi waliyonayo ambayo inaweza kuifanya
Tanzania ikawa na timu nyingi zaidi kwenye michuano ya kimataifa lakini
hiyo watu hawaiangalii, ukiangalia maandalizi ya mechi ya Yanga na Rayon
Sports haikuwa na uzito kama mechi ya Yanga na Simba wakati kwa fedha
na nafasi ya nchi kuwa na timu nyingi kimataifa ilikuwa ni mechi muhimu
sana.”
“Zambia sasa hivi inawakilishwa na timu nne kwenye mashindano ya
kimataifa kwa sababu ZESCO ilifika hadi nusu fainali, kwa mtazamo wangu
kwa kundi ambalo Yanga ilipangiwa nikitarajia haya TFF waiongezee
wachezani hata kutoka maeneo mengune kama ambavyo waliwahi kufanya ili
Yanga ifike angalau nusu fainali nchi itanufaika kwa kupata nafasi nne
jambo ambalo litaifaidisha nchi.”
“Kundi ambalo Yanga imepangwa ingekuwa watu wanaojipanga ungekuwa
mwaka wa kuongeza tumu kwenye mashindano ya kimataifa lakini unaweza
ukashangaa sisi tusitumie hiyo fursa lakini ingekuwa Zambia wamepangwa
kundi hili wangefika nusu fainali.”
No comments