Full-Width Version (true/false)


Waziri Mwijage ampa ushauri huu rapa Chemical baada ya kutazama ngoma yake mpya ‘Africa’s Heritage’Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amemshauri msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Chemical kwa kumtaka abadilishe jina lake baada ya kutazama wimbo wake mpya wa ‘Africa’s Heritage’.

Mwijage amefunguka hayo leo Mei 30,208 akiwa katika maonesho ya wiki ya maonesho ya utafiti yanayoendelea katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Chemical alitambulishwa kwa Waziri Mwijage chuoni hapo na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Kitivo Cha Urithi wa Utamaduni, Dkt. Eldidius Ichumbaki ambapo huwa wanamtumia kupitia kazi zake za kisanii kutangaza vivutio vinavyopatikana Tanzania.

Hukuona majina yote hadi ukaamua kujiita Chemical? kusema kweli mimi jina hilo kwangu halijakaa vizuri na hii kazi unayoifanya hapa Chuo Kikuu, nitakutafutia jina lingine si utaniruhusu?,” amemaliza Waziri Mwijage kwa kumuuliza swali Chemical hii ni baada ya kutazama video hiyo ya Africa’s Heritage.

No comments

Powered by Blogger.