Full-Width Version (true/false)


Waziri Ummy amkingia kifua Mbunge Goodluck Mlinga kuhsu kuchoma sindanoWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa uchomaji wa sindano una taratibu zake huwezi kujichomea sindano ovyo ovyo.

Kauli hiyo inakuja mara baada ya Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga kusambaa video ikionyesha anazindua chanjo ya watoto ambayo alionekana ameshika sindano na anamchoma mwanafunzi wa kike.

“Nataka kukiri kwamba uchomaji wa sindano una taratibu zake huwezi kujichomea sindano ovyo ovyo, Mh. Asunta Mshama Mkuu wa Wilaya ya Kibaha na Mh. Goodluck Mlinga hawakuwachoma chanjo watoto husika ila walifanya kama demostretion,” amsema Waziri Ummy.

“Kwa waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuzingatia miongozo ya utoaji wa huduma za afya kwasababu hata kitendo cha kushika sindano kama sio mtaalam sio kitendo cha kitaaluma kwahiyo tulishakemea na Mganga Mkuu wa serikali atatoa tamko rasmi kwahiyo wabunge mimi niendelee kuwahimiza wazazi na walezi kupeleka watoto kupata chanjo kwasababu chanjo hii ni kwasababu ya maendeleo yao.”

Hata hivyo Mbunge huyo kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika hivi “Hili halikuwa tukio la kweli, ilikuwa kwa ajili ya kupiga picha tu.”

No comments

Powered by Blogger.