Full-Width Version (true/false)


Waziri wa Afya afunguka kuhusu picha inayosambaa ya Mbunge akimchoma sindano mwanafunziPicha inayosambaa ikimuonesha Mbunge wa Ulanga Goodluck Milinga akimchoma sindano mwanafunzi
Baada ya picha ya Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga kusambaa kwenye mitandao ya kijamii akimchoma sindano mwanafunzi kama ishara ya kuzindua chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi wilayani Ulanga, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto ,Ummy Mwalimu ameibuka na kusema kuwa kitendo hicho si sahihi.

Waziri Ummy Mwalimu ameyasema hayo baada ya watumiaji mbalimbali wa mitandao ya kijamii kulaani kitendo hicho huku baadhi wakisema ni kucheza na afya za watu, kutokana na mtu asiye na utaalamu wa kitabibu kufanya shughuli hiyo.


Waziri Mwalimu amesema kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya atoe maelekezo ili kuhakikisha kuwa kanuni za kitabibu zinazingatiwa.

"Hii sio sahihi. Tayari nimeshamuelekeza Katibu Mkuu Afya kutoa maelekezo mara moja kwa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kusisitiza uzingatiwaji wa Miongozo ya kitaalamu yafanywe na Wataalamu".Ameadika Ummy MwalimuNo comments

Powered by Blogger.