Waziri wa Nishati Amuomba Mungu Ailaze Serikali Mahali Pema Peponi
Waziri
wa Nishati, Dk. Medard Kalemani amewavunja mbavu wabunge baada ya
kuwaambia anamuomba Mwenyezi Mungu aiweke serikali mahala pema peponi.
Dk.
Kalemani ametoa kauli hiyo bungeni jijini Dodoma leo Mei 25, alipokuwa
akihitimisha mjadala wa Bajeti ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/19
aliyowasilisha jana.
Kabla
ya kusema hayo Dk. Kalemani alikuwa akieleza jinsi serikali
ilivyotekeleza miradi mbalimbali na kuwapelekea wananchi umeme katika
maeneo mbalimbali nchini ambapo alijikuta akisema: “namuomba Mwenyezi
Mungu aiweke serikali mahali pema peponi,”.
Hatua
hiyo iliwafanya wabunge kuangua vicheko huku Mwenyekiti wa Bunge, Mussa
Zungu akilazimika kuwatuliza wabunge na kuwataka waendelee kumsikiliza
waziri badala ya kucheka.
Hata
hivyo, baada ya dakika chache Dk. Kalemani alisema anamuomba Mwenyezi
Mungu aibariki serikali na kuwafanya wabunge kucheka tena kwa sauti.
No comments