Waziri, wanasaikolojia wazungumzia kukithiri matukio ya watu kujiua
Kwa kawaida binadamu hukiogopa kifo, lakini maswali huibuka pale
anapoamua kujitoa uhai.
Katika
siku za hivi karibuni kumekuwa na mfululizo wa matukio ya watu kujiua, ambapo
ndani ya mwezi mmoja, wanne wameripotiwa kujitoa uhai nchini.
Katika
tukio la jana, mganga mfawidhi wa Kituo cha Afya Kakonko, mkoani Kigoma, Mejo
Banikira (43) alikutwa amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia taulo.
Kabla
ya tukio la Banikira, Mei 6, mwanafunzi wa kidato cha sita wa Shule ya
Sekondari Kahororo iliyopo wilayani Bukoba, Robert Masaba alijinyonga zikiwa
zimesalia saa chache kabla ya kufanya mtihani wa mwisho.
Siku
nne baadaye mwanafunzi wa mwaka wa pili Chuo Kikuu cha Makumira mkoani Arusha,
Luciana Richard (25), mkazi wa Morogoro alijinyonga akiwa chumbani kwake kwa
kile kilichodaiwa kuwa ni msongo wa mawazo.
Tukio
hilo lilitokea katika Kitongoji cha Kilalanaiti, Kijiji cha Ndatu, Kata ya
Pori. Mwanafunzi huyo alijinyonga kwa kutumia mtandio alioufunga juu ya mlango
wa bafu.
Mei
27, 2018, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha St Augustine (Saut) tawi la Mbeya, Moses
Mashaka alikutwa amekufa ikidaiwa alijinyonga chumbani kwa kutumia shuka.
Wakati
matukio hayo yakiendelea kujitokeza, Januari ripoti ya Shirika la Afya Duniani
(WHO), iliitaja Tanzania kushika nafasi ya 27 barani Afrika kwa vifo
vinavyotokana na watu kujiua.
Kwa
upande wa Afrika Mashariki, ripoti hiyo inaonyesha kuwa Tanzania inashika
nafasi ya nne kwa kuwa na idadi kubwa ya wanaojiua.
Katika
ukanda huo, Rwanda inaongoza kwa kuwa na asilimia 8.5 ya vifo vya kujiua
ikifuatiwa na Burundi yenye asilimia nane.
Nafasi
ya tatu inashikiliwa na Uganda kwa kuwa na asilimia 7.1 huku Tanzania
ikishikilia nafasi ya nne kwa kuwa na asilimia saba.
Naibu
waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine
Ndugulile alitaja chanzo cha matukio hayo kuwa ni pamoja na uelewa mdogo wa
jamii wa kukabiliana na msongo wa mawazo hatua inayosababisha baadhi ya watu
kuchukuliwa hatua za kisheria kwa makosa ya majaribio ya kujiua.
“Kabla
ya kuchukua uamuzi huo ziko hatua, eneo mojawapo ni sonona (depression), hii ni
hatua inayosumbua wengi kwa mfano huzuni ya kwenye mgogoro wa mapenzi na kwa
bahati mbaya (mtu) asipate mshauri wa karibu,”alisema.
Dk
Ndugulile alisema idadi ndogo ya watalaamu wa saikolojia nchini ni sehemu ya
changamoto ya jamii kukosa msaada wa ushauri na Serikali inahitaji kuongeza
nguvu zaidi katika kushughulikia wagonjwa wa sonona.
Wanasaikolojia
wanasemaje?
Wanasaikolojia
wanasema binadamu hufikia hatua ya kujiua baada ya akili kukosa uwezo wa
kuhimili uzito wa changamoto anazokabiliana nazo.
Mwanasaikolojia
Charles Nduku alisema maeneo mawili yanayochagiza kuwapo kwa idadi kubwa ya
vifo vya aina hiyo ni kutotimiza malengo na matarajio ambayo mtu hujiwekea
pamoja na presha za kimaisha kuzidi uwezo wa kufikiri.
Nduku
alisema uamuzi huo hutokea dakika chache baada ya mtu kukutana na changamoto
inayozidi uwezo wake wa kupata mbadala. Alisema akili ya mtu anayetaka
kutekeleza tukio hilo kwa wakati huo huwa imefungiwa katika suluhisho hilo
pekee kama njia ya kuyakimbia matatizo.
“Asili
ya tatizo liwe kubwa au dogo halimfanyi mtu kujiua ila uwezo wake wa kuhimili
tatizo hilo, anajiuliza kwa nini mimi, kwa nini nisife tu? Sasa ukimuwahi
dakika tano kabla ya kufanya uamuzi huo ukamwambia kuwa yeye ni wa thamani,
anaweza kubadili uamuzi huo palepale,” alisema.
“Mara
nyingi matukio ya kujiua yanahusisha kundi la mapenzi kwa sababu watu wanaishi
kwa hisia zaidi, lakini ukikuta anayeishi kwa kutafakari siyo rahisi kuchukua
uamuzi huo.”
Kwa
bara la Afrika, Equatorial Guinea inaongoza kwa wingi wa vifo vinavyotokana na
watu kujiua kwa kuwa na asilimia 22.6 ikifuatiwa na Angola yenye asilimia 20.5
na ya tatu ni Ivory Coast yenye asilimia 18.1.
Mwanafunzi,
daktari
Mwanafunzi
wa Saut alijiua kwa kujinyonga na shuka chumbani kwake katika mtaa wa
Maendeleomjini Mbeya.
Mshauri
wa wanafunzi chuoni hapo, Daud Kapufi alisema baada ya uchunguzi wa daktari,
polisi walitoa ruhusa kwa familia kuuchukua mwili. Mwili huo umesafirishwa
kuelekea Geita kwa mazishi.
Naye
Dk Banikira alikutwa amejinyonga chumbani kwake akiwa na miezi isiyozidi minane
tangu alipohamishiwa Kakonko kutokea Simanjiro.
Kwa
mujibu wa majirani, mtaalamu huyo wa afya alikuwa akiishi peke yake katika
makazi hayo.
No comments