Full-Width Version (true/false)


WCB walimruhusu Rayvanny kumuimba Alikiba, mwenyewe aeleza ilivyokuwa

 

Msanii wa muziki Bongo kutoka WCB, Rayvanny amesema label hiyo ilimpa baraka zote kutaja jina la Alikiba katika ngoma yake ‘Natafuta Kiki’.
Rayvanny anayefanya vizuri na ngoma ‘Pochi Nene’ ameiambia The Playlist ya Times FM kuwa msanii ili kutoka muziki mzuri hatakiwi kijiwekea mipaka katika utunzi wake.

“Niliongea nao wakaniambia fresh kwa sababu nao wanajua tunafanya kazi ya sanaa, tunawakilisha jamii kwa hiyo kitu ambacho unakifanya ukijibanana unaweza ukatoa wimbo mbaya kwa sababu uliogopa kuweka neno fulani,” amesema Rayvanny.

WCB ni label ya Diamond Platnumz ambaye anatajwa kuwa mshindani mkubwa wa Alikiba.

Utakumbuka mwaka 2016 Alikiba aliingia katika mzozo mkubwa na meneja wa Diamond, Sallam SK kwa kile alichodai meneja huyo alimfanyia ‘figisu’ kwenye tamasha la Mombasa Rocks Music [Festival].

No comments

Powered by Blogger.