Full-Width Version (true/false)


Wema Sepetu aeleza sababu za kushindwa kufika kwenye uzinduzi wa filamu ya Aunt EzekielMalkia wa filamu Bongo, Wema Sepetu ameeleza sababu ya kushindwa kuhudhuria kwenye uzinduzi wa filamu fupi ya dakika 20 ‘MAMA’ ya Aunt Ezekiel iliyofanyika usiku wa jana (Jumapili) Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Madam Sepenga ametoa taarifa hiyo kupitia kwenye mtandao wa Instagram akidai kuwa alichelewa kutokana na Mama yake ndio alimchelewesha na kujikuta ameshindwa kufika kwenye uzinduzi huo.

“I was soooo Ready for MAMA Short Film But My MAMA Took my Time aswell… Nikachelewa…,” ameandika Wema kwenye mtandao huo.

Hata hivyo Aunt Ezekiel alipohojiwa na Mwananchi Digital sababu za Wema Sepetu kushindwa kufika katika uzinduzi huo alisema ni kutokana na gauni la mrembo huyo alilotakiwa kuvaa kwenye uzinduzi huo lilikuwa bado lipo kwa fundi halijamalizika kwa sababu ya kukatika kwa umeme.

No comments

Powered by Blogger.