Full-Width Version (true/false)


Wema Sepetu apelekwa India kwa matibabu

Mwanadada muigizaji wa filamu nchini Wema Sepetu anayekabiliwa na kesi ya matumizi ya dawa za kulevya ameshindwa kufika mahakamani leo na kudaiwa kuwa yupo Nchini India kwa matibabu. 
Hayo yameelezwa na Mama mzazi wa Wema, Mariam Sepetu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa serikali Constantine Kakula kuhoji kwanini Wema hakufika mahakamani ambapo wakili alishangazwa na taarifa hizo na kudai kuwa hakuna uthibitisho wowote wa kuonyesha Wema anaumwa, hivyo anaiomba mahakama isimamie sheria.

Baada ya kutoa maelezo hayo Mama Wema akatoa nyaraka za binti yake za kusafiria na kuieleza mahakama kuwa Wema anaumwa na amekwenda nchini India kufanyiwa upasuaji.

Kutokana na hoja hiyo, Hakimu Simba amesema ni kweli hakuna uthibitisho, hivyo katika tarehe ijayo uthibitisho unapaswa kuwepo, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi June 13,2018.

No comments

Powered by Blogger.