Full-Width Version (true/false)


Wema Sepetu na wasanii wengine wateuliwa kuwa mabalozi wa Kombe la Dunia

Kampuni ya StarMedia rasmi imezindua kuonyesha mechi 64 za Kombe la Dunia, michuano itakayofanyika nchini Russia.

Michuano hiyo itaanza Juni 15 nchini Russia na mechi zote 64 zitaonyeshwa kupitia king’amuzi cha StarTimes kilicho chini ya kampuni ya StarMedia.

Wakati wa uzinduzi huo, Startimes walimtangaza rasmi mwigizaji maarufu nchini, Wema Sepetu  kuwa kiongozi wa kundi la wasanii ambao watakuwa mabalozi wao wakati wa michuano hiyo.

Mabalozi hao ni pamoja na wasanii wengine maarufu kama Hamad Ally maarufu kama Madee, msanii Man Fongo, Mkali Wao, Ibitoke, mwigizaji Monalisa, Mkude Simba na wengine ambao watafanya kazi ya ubalozi.

Pamoja na hivyo, michuano hiyo itarushwa kwa lugha ya Kiswahili kutoka nchini Russia.

Startimes imepanga kurusha michuano hiyo kwa Kiswahili ili kuisogeza kwa Watanzania zaidi.

No comments

Powered by Blogger.