Full-Width Version (true/false)


Wizara ya Afya yapiga marufuku madaktari kumiliki zahanati

 

 
Wizara ya Afya imepiga marufuku Madaktari bingwa kumiliki Zahanati nchini Tanzania,

Taarifa iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Pamella Sawa, imewataka Waganga Wakuu wa Mkoa na Wilaya kutopitisha maombi ya kufungua Zahanati yanayowasilishwa na Madaktari Bingwa,

Taarifa hiyo ilisema Madaktari hao Bingwa wamekuwa wanatumia Zahanati zao kutoa huduma zinazostahili kutolewa kwenye vituo vya ngazi za juu,

Alizitaja baadhi ya huduma hizo kuwa ni pamoja kufanya upasuaji mkubwa ambao haustahili kufanywa kwenye Zahanati,

Taarifa iliwaelekeza Madaktari Bingwa kufungua Kliniki za  Kibingwa na kuendelea. Lakini pia taarifa hiyo iliwataka Madaktari Bingwa wanaomiliki Zahanati, wazibadilishe ili ziwe Kliniki za Kibingwa,

No comments

Powered by Blogger.