Wizara ya fedha yashtakiwa

Mbunge wa Tandahimba (CUF), Katani Ahmadi ameliomba Bunge kuchukua hatua kali dhidi ya Wizara ya Fedha na Mipango ambayo imekuwa ikilalamikiwa kwa kutokutoa fedha zinazopitishwa na mhimili huo.
Katani
amesema miradi mingi imekuwa ikishindwa kutekelezwa kutokana na wizara
ya fedha kushindwa kutoa fedha licha ya Bunge kuzipitisha.
Amesema wakandarasi wa Rea wameshindwa kutekeleza usambazaji wa umeme
kwa kukosa fedha ambazo zilipitishwa na Bunge huku mawaziri
wakinyooshewa vidole kwa makosa ambayo si ya kwao.
“Sijui wizara ya fedha tufanye jambo gani, tumeona katika kilimo, fedha za korosho hakuna sijui kuna jinsi gani wizara ya fedha,” ameongeza
Katani amesema hakuna mpinzani nchini si mzalendo au kupinga miradi
yenye tija kwa taifa lakini wanayozungumza Serikali inapaswa
kuyasikiliza na kuyafanyia kazi.
“Sisi sote ni wazalendo tunachokisema mtumie hekima za
pamoja, mawaziri msikilize yanayosemwa, kama haya mnaambiwa katika
Stiegler’s Gorge mkubali tunayosema, kwamba tathimini iko wapi,
ilifanyika lini, tukisema mnasema sio wazalendo, Tunaposhauri
tunashauri na nia nzuri, hatuna tatizo na CCM, tuna tatizo na matendo ya
CCM, tukisema mnaanza kusema nini,” amesema Katani
No comments