Full-Width Version (true/false)


Yanga ijiandaa kupapaswa - Masau Bwire

Uongozi wa timu ya Ruvu Shooting umefunguka na kuitaka Klabu ya Yanga na wawakilishi pekee Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa, kujiandaa kisaikolojia katika kupokea matokeo ya kufungwa kwenye mchezo wa Mei 25, 2018 wanapokutana dimbani. 
Hayo yamebainishwa na Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire wakati alipokuwa anazungumzia maandalizi ya kuelekea mchezo huo kupitia kipindi cha Kumekucha Michezo kinachorushwa mubashara kutokea ITV na kusema watatumia mechi hiyo kuwaonesha watanzania uwezo waliokuwa nao Ruvu Shooting kwa sasa.

"Yanga wanatakiwa kujipanga kisaikolojia katika hali ya kupokea matokeo ambayo tumeyapanga kuwapa siku ya Ijumaa, hilo tumelidhamiria. Tangu tuanze mfumu huu wa kupapasa kwa kweli tunapapasa hatutanii", amesema Bwire.

Ruvu Shooting FC inashuka dimbani ikiwa imeshika nafasi ya nane kwa alama 36 huku ikicheza michezo 28 huku Yanga yenyewe ikiwa nafasi ya tatu kwa alama 51 ikicheza michezo 28 pekee tokea ligi kuanza.

No comments

Powered by Blogger.