Full-Width Version (true/false)


Yanga kufanya maamuzi magumu kuhusu Donald Ngoma.

Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Usajili, Hussein Nyika, umesema kuwa utafanya mamuzi magumu kuhusiana na mchezaji wake, Donald Ngoma.
Akizungumza asubuhi na Radio EFM asubuhi hii, Nyika, ameeleza kuwa uongozi utakaa na kujlijadili suala la Ngoma na baadaye utaweza kuja na maamuzi ambayo watayatangaza.

Ngoma amekosekana kwa muda mrefu Uwanjani kutokana na kusumbuliwa na majeraha tangu msimu wa ligi uliopita.

Mbali na maamuzi hayo kwa Ngoma, Yanga wamesema watafanya mabadiliko makubwa katika kikosi chao kwa ujumla kutokana na namna kiwango cha timu kilivyo kwa ujumla.

Kauli hizo zimekuja kufuatia kipigo cha mabao manne kwa sifuri dhidi ya USM Alger kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika usiku wa jana.

No comments

Powered by Blogger.