Full-Width Version (true/false)


Yanga kujitetea mbele ya Azam FC


Klabu ya soka ya Yanga leo itashuka kwenye dimba la Jamhuri mjini Morogoro dhidi ya Mtibwa Sugar ikiwa ni mechi yake ya 26 na itakuwa na kazi ya kujaribu kuitoa Azam FC katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi. 
Yanga ambayo ipo katika nafasi ya tatu inaingia uwanjani leo ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mcheoz wake ulopita dhidi ya Tanzania Prison na kuwafanya wavuliwe rasmi taji ligi kuu walilokuwa wakilishikilia kwa misimu mitatu mfululizo.

Azam FC ipo juu ya Yanga kwa alama 4 ikiwa na alama 52 Yanga ikiwa na alama 48 hivyo ikishinda leo itafikisha alama 51 huku ikiwa imetanguliwa mechi 2 na Azam FC ambayo hadi sasa imeshacheza mechi 28.

Pia Yanga inaweza kuchezesha kikosi cha wachezaji ambao hawapati nafasi kwenye kikosi kama ilivyokuwa kwenye mechi ya Tanzania Prison, kutokana na kukabiliwa na mchezo wa Kombe la shirikisho dhidi ya Rayon Sports.

Yanga SC itarejea jijini Dar es Salaam kesho, baada ya mchezo wa leo, kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya Kundi D Kombe la Shirikisho dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda utakaopigwa Mei 16 uwanja wa taifa.
 

No comments

Powered by Blogger.