Full-Width Version (true/false)


Yanga kukiamsha keshoKikosi cha wawakilishi pekee kwenye mashindano ya Kombe la shirikisho Barani Afrika Yanga SC kinatarajiwa kuondoka Jijini Dar es Salaam alfajiri ya kesho Mei 18, 2018 kuelekea Mkoani Shinyanga, tayari kwa mchezo wa ligi kuu Mei 19 dhidi ya Mwadui FC. 
Hayo yamewekwa wazi na taarifa zilizotolewa na uongozi wa Yanga na kusema msafara huo utajumuisha wachezaji 20 pamoja na safu ya viongozi nane pekee.

Timu ya Yanga inaifuata Mwadui FC mkoani Shinyanga kukamilisha ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuwa mpaka sasa klabu ya Simba SC imeweza kujitangazia ubingwa wa VPL msimu huu wa mwaka 2017/18 kwa kuweza kufikisha 68 ambazo haziwezi kufikiwa na Azam FC wala Yanga SC ambao ndio wapo nyuma ya Simba kwa mujibu wa msimamo wa Ligi kuu Tanzania Bara.

No comments

Powered by Blogger.