Full-Width Version (true/false)


YANGA KUSHINDA MECHI ZOTE ZILIZOBAKI ILI KUZIMA KELELE ZA UBINGWA SIMBA

Baada ya kusalimu amri kwa kuipa nafasi Simba ya kuutwaa ubingwa wa ligi msimu huu, Yanga wamesema watapambana kushinda mechi zote zilizosalia.

Kupitia kwa Afisa wa Habari wa Yanga, Dismas Ten, ameeleza kuwa Yanga inahitaji heshima ya kushinda mechi zote zilizosalia ili kulinda heshima yao.

Ten anaamini ushindi wa mechi zilizosalia utathibitisha kuwa wao ndiyo mabingwa wa taji la ligi mara tatu mfululizo pamoja na kuweka heshima ya kuonesha kuwa wao si wasindikizaji.

Kikosi cha timu hiyo kipo Mbeya muda huu tayari kwa mchezo dhidi ya Tanzania Prisons utakaoanza majira ya saa 10 kamili jioni.

Yanga imeenda Mbeya ikiwa na wachezaji pungufu huku ikiwa na dhamira ya kuwapunguza Simba shamrashamra za ubingwa kwa kuhakikisha kuwa inapata alama tatu muhimu.

No comments

Powered by Blogger.