Full-Width Version (true/false)


Yanga tena kwa mara ya 9Klabu ya Yanga imeambulia kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wenyeji Mwadui FC jioni ya leo kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, ikiwa ni mwendelezo wa ligi soka Tanzania Bara. 
Klabu hiyo sasa imecheza mchezo wa 9 bila kupata ushindi katika mashindano yote tangu aliyekuwa kocha wao George Lwandamina aondoke na kurejea kwao Zambia.

Yanga ambayo ilikuwa inacheza mchezo wa 27 kwenye ligi kuu msimu huu na kubakiza mechi tatu, imekubali kipigo hicho kwa bao la Awesu Ally aliyefunga dakika ya 19.

Kwa upande mwingine Yanga imepokea kichapo cha tatu mfululizo kwa mara ya kwanza katika misimu minne ya ligi kuu iliyopita ambapo ilianza kwa kufungwa na Simba 1-0, ikafungwa na Prison 2-0 na leo 1-0 dhidi ya Mwadui FC.

Yanga sasa imebaki kwenye nafasi yake ya 3 ikiwa na alama 48 nyuma ya Azam FC yenye alama 52 huku Simba ambayo imetwaa ubingwa ikiwa na alama 68 baada ya leo kufungwa na Kagera Sugar.

No comments

Powered by Blogger.