Full-Width Version (true/false)


Yanga waondoka kinyonge kwenda Algeria

Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga wameondoka nchini kwenda Algeria kuivaa USM Alger katika mechi ya Kombe la Shirikisho.

Mechi hiyo itapigwa Jumapili lakini Yanga wameondoka katika hali inayoonyesha hawakuwa na morali.

Jana kulikuwa na mgomo baridi wakidai malipo yao, lakini uongozi ukajitahidi kukanusha kwa kuwa kuna baadhi ya wachezaji wamegoma kuondoka na timu.

Kocha Mwinyi Zahera raia wa DR Congo naye alikuwa sehemu ya msafara huo pamoja na wasaidizi wake.

No comments

Powered by Blogger.