Full-Width Version (true/false)


YANGA WAONDOKA KUELEKEA MBEYA, WALIOBAKI WAONGEZEKA
Kikosi cha Yanga kimeondoka leo kuelekea Mbeya kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa kesho Alhamis.

Yanga imeondoka mapema leo asubuhi kuelekea jijini humo huku ikielezwa kuwa kipa namba moja wa Yanga, Youthe Rostand ni miongoni mwa wachezaji waliosalia Dar es Salaam.

Haijajulikana sababu za mchezaji huyo kubaki Dar es Salaam na uongozi haujataja idadi rasmi ya wachezaji ambao wamesafiri kwa ajili ya mechi hiyo dhidi ya Tanzania Prisons.

Mbali na Rostand, wapo baadhi waliosalia Dar es Salaam wakiungana na baadhi ya walioshindwa kusafiri na timu kuelekea Algeria kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger.

Yanga itakuwa mgeni kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ambapo mchezo huo utaanza majira ya saa 10 kamili jioni.

No comments

Powered by Blogger.