Full-Width Version (true/false)


Yanga yaingia sokoni kusaka vifaa 3 kimataifa

Waada ya kutoka sare ya kutofungana katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi kombe la shirikisho Afrika dhidi ya kikosi cha Rayon Sports ya Rwanda, uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kusajili wachezaji watatu wa kigeni.

Katibu mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa amethibitisha hilo, kwa maana hiyo mchakato wa kumpata mshambuliaji Adam Salamba kutoka Lipuli FC umwpigwa chini rasmi.

“Tunafanya mchakato wa kuziba nafasi muhimu zenye upungufu ili kuboresha zaidi kwa sababu tunaimani njia bado ipo na tutapambana kuhakikisha tunapata matokeo mazuri.”

“Kabla hata ya kwenda kwenye mashindano ya SportPesa tutatangaza kikosi chetu ambacho kitakuwa na wageni kadhaa hatuwezi kuwataja kwa sababu tukiwasema sasa hivi watu wengine wanazunguka nyuma kwenda kutuponda na wanawasajili kwa hiyo tumeona tusitaje ni akina nani ili muda ukifika watu watajulishwa ni akina nani tutakaowaongeza.”
“Tutaongeza wachezaji watatu wote kutoka nje.”

Mkwasa amesema matokeo ya suluhu katika mechi nyingine ya Kundi B kati ya Gor Mahia na USM Alger yanafanya nafasi kuwa wazi katika kundi hilo kama watapata matokeo kwenye mechi zao zijazo.

“Nafasi na fursa bado kwa hiyo cha kufanya ni kujipanga vizuri ili kupata matokeo mazuri kwa sababu kama jana tungepata matokeo tungekuwa kwenye nafasi nzuri.”

No comments

Powered by Blogger.