Full-Width Version (true/false)


Yanga yaomba msaadaUongozi wa klabu ya Yanga SC umewasilisha maombi kwa klabu ya Lipuli FC ya Iringa kwaajili ya kumchukua kwa mkopo mshambuliaji, Adam Salamba ili aongeze nguvu kwenye kikosi hicho katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. 
Katibu Mkuu wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa ameweka wazi hilo na kusema kuwa kwa sababu kanuni zinawaruhusu kuongeza wachezaji baada ya kuingia hatua ya makundi, wanataka kumsajili Salamba.

“Tayari tumewaandikia barua Lipuli FC kumuomba Adam Salamba kwa ajili ya Kombe la Shirikisho Afrika,”amesema Mkwasa. Mbali na Salamba, inasemekana pia Yanga SC  inamtaka mshambuliaji wa Mbao FC ya Mwanza, Habib Kiyombo.


Adam Salamba amekuwa nguzo muhimu kwa klabu ya Lipuli FC msimu huu ambao ni wa kwanza kwa timu hiyo iliyopanda daraja msimu uliopita. Katika michuano hiyo kundi D lina timu za U.S.M Alger, Gor Mahia, Rayon Sports na Yanga.

Yanga ilianza vibaya michuano ya Kombe la Shirikisho kwa kufungwa mabao 4-0 na wenyeji, U.S.M. Alger katika mchezo wake wa kwanza wa Kundi D Kombe la Shirikisho Jumapili iliyopita.

No comments

Powered by Blogger.