Full-Width Version (true/false)


Yanga Yarejea Kimya Kimya DarKIKOSI cha Yanga kimewasili Dar leo (Jumanne) Mei 8, 2018 kikitokea Algeria ambako kilicheza mchezo wake wa kwanza wa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger na kupoteza mchezo huo kwa kufungwa 4-0.

Baada ya kurejea nchini, Yanga inakabiliwa na mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara (Vodacom Premier League – VPL)  dhidi ya Tanzania Prisons Alhamisi ya Mei 10, 2018,  mchezo ambao unatarajiwa kuchezwa uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Ikitoka mkoani Mbeya, Yanga itacheza mechi nyingine ya VPL dhidi ya Mtibwa Sugar Mei 13, 2018 kwenye uwanja wa Jamhuri mkoni Morogoro kabla ya mchezo wao wa kimataifa dhidi ya Rayon Sports Mei 16, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa.

No comments

Powered by Blogger.