Full-Width Version (true/false)


Yanga yatangaza kiama kimataifaKlabu ya Mabingwa Watetezi Ligii Kuu Tanzania Bara na wawakilishi pekee nchini Tanzania katika mashindano ya kimataifa Yanga, wanatarajia 'kukwea pipa' kesho Mei 3, 2018 kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wao wa kwanza hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho dhidi ya wenyeji U.S.M Algers.
Hayo yamethibitishwa na taarifa zilizotolewa na Meneja wa timu kupitia ukurasa maalum wa Yanga, Hafidh Saleh na kusema kwamba matayarisho ya mchezo huo yanakwenda vizuri hadi sasa

"Tuko sawa tumejiandaa, tunahitaji kupata matokeo mazuri, ili kujenga ari mpya katika adhma yetu ya kufanya vizuri kimataifa, hatua ya makundi ni ngumu kwa sababu kila mchezo unakutana na timu ngumu. Nia yetu msimu huu tufike mbali zaidi kuliko miaka yote iliyopita", amesema Saleh.

Yanga ilifanikiwa kutinga hatua ya makundi baada ya kuitoa Wolayta Dicha ya Ethiopia kwa jumla ya ushindi wa mabao 2-1. Mechi za hatua ya makundi zinatarajiwa kuanza Mei 4 na 6.

No comments

Powered by Blogger.