Full-Width Version (true/false)


Yanga yatoa onyo kwa baaadhi ya timu zinazotaka kusajili wachezaji wake kinyemela

 

Uongozi wa klabu ya Yanga umetoa onyo kwa timu zinazotaka kuwasajili wachezaji wake kwa njia za kinyemelea kuacha mara moja na badala yake zifuate taratibu.


Ofisa wa Habari wa klabu hiyo, Dismas Ten, amesema kuwa kama kuna timu inahitaji kufanya usajili kutoka kwao basi ifuate taratibu rasmi kwa kuzingatia kanuni za usajili.


Ten ameeleza hayo kupitia kipindi cha michezo cha Radio EFM wakati akizungumzia namna wanavyojipanga kuanza maandalizi ya michuano ya SportPesa Super Cup inayotaraji kuanza Juni 10 2018 nchini Kenya.


Mkuu huyo wa kitengo cha habari ndani ya Yanga ameeleza kuwa ni vema kama klabu inahitaji mchezaji kutoka Yanga ikawasili kwenye makao yao makuu kufanya nao mazungumzo ili waweze kufikia mwafaka wa makubaliano juu ya mchezaji husika anayehitajika.


Michuano ya SportPesa Super Cup itaanza Juni 3 mpaka 10 2018 jijini Nairobi huko Kenya na itahusisha timu zote zilizo chini ya udhamini wa kampuni hiyo ya bahati nasibu.

No comments

Powered by Blogger.