Full-Width Version (true/false)


Yanga yaungana na Man United
Klabu ya soka ya Yanga imeungana klabu ya soka ya Manchester United na mashabiki wengine wa soka duniani kumuombea apone haraka kocha wa zamani wa Man United Sir Alex Ferguson ambaye amefanyiwa oparesheni ya Ubongo.

Kocha huyo mwenye mafanikio makubwa ndani ya United na ligi kuu ya England, jana alifanyiwa upasuaji wa Ubongo (Brain haemorrhage) na kwa mujibu wa klabu yake hiyo ya zamani upasuaji ulienda salama.

Yanga kupitia ukurasa wao wa Instagram wameandika, ''Tunaungana na wapenda soka duniani kote, kukutakia heri na kukuombea urejee kwenye afya njema'', ambapo ujumbe huo umeambatana na picha ya Fergie.


Kwa upande wao Manchester United wamesema upasuaji umefanyika salama kabisa ila kwasasa bado yupo Hospitali kwa mapumziko zaidi chini ya uangalizi wa jopo la madaktari.

No comments

Powered by Blogger.