Full-Width Version (true/false)


Young Killer amponda Stamina baada ya kuoa

 Msanii Young Killer Msodoki ameonesha kutofurahishwa na kitendo cha rapper Stamina kwenda kufannya show siku ya harusi yake, akisema kwamba jambo hilo hajalipokea kwa mikono miwili kabisa kama rafiki. 
Akizungumza kwenye eNewz ya East Africa Television, Young Killer amesema siku ya harusi ni siku maalum kwa mtu kupumzika na mwenza wake kwa kuwa wameanza ukurasa mpya kwenye maisha ya mahusiano, hivyo haikuwa kitu kizuri kwani show bado zipo na atazikuta.

“Ni jambo ambalo kwa haraka haraka unaweza ukalipokea katika hali ya ugumu sana, siku ya kufunga ndoa inakuwa special sana, ni siku ambayo inabidi uwe unatulia na mwenzako mkitoka ukumbini, kwamba huu ndio mwanzo wetu, binafsi ni jambo ambalo sikulipokea vizuri kutokana na ile ni siku special, na show kila siku bado zipo na tunazifanya, ukitoka kufanya harusi inabidi ukapumzike na mwenza wako”, amesema Young Killer

Kwa upande wake amesema iwapo yeye atafikia kufunga ndoa hatofanya jambo hilo, isipokuwa ataenda kujifungia na mwenza wake ili kufurahia siku hiyo muhimu kwenye maisha yake.

No comments

Powered by Blogger.