Full-Width Version (true/false)


Zamaradi alimaliza sakata la rambirambi ya Masogange

Sakata la pesa ya rambirambi za aliyekuwa video vixen, Agnes Masogange linaendelea kufukuta kila kukicha lakini mtangazaji, Zamaradi Mtetema amekuja kulimaliza.

Steve Nyerere ambaye alikuwa mratibu wa msiba huo, aliingia matatani baaada ya familia ya marehemu kudai hawajapata rambirambi iliyobaki.

Mwigizaji huyo alibanwa kila kona kwa madai kuwa ametia kapuni salio la rambirambi ambalo lilipangwa apewe mtoto wa marehemu aitwaye Sania.

Baada ya tetesi hizo Steve kuibuka kukanusha tuhuma hizo, huku mtangazaji mashuhuri Zamaradi Mketema naye aliibuka kumtetea akisema fedha zilizobaki anazo yeye.

Kwa mujibu wa mtandao wa gazeti la Mwananchi limedai, Mketema amesema fedha hizo anazo na familia ya marehemu inafahamu huku ikisubiriwa utaratibu wa kumfungulia akaunti benki ili wamuewekee kwa ajili ya kupa ada atakapoanza kidato cha kwanza mwakani.

No comments

Powered by Blogger.