Full-Width Version (true/false)


Zari awapa somo wanawake wanao danga

 
Zari azidi kumkumbuka aliyekuwa mzazi mwenzake Marehemu Ivan Don kupitia ukurasa wake wa instagram na kuwapa ushauri wanawake wanaowategemea wanaume katika maendeleo yao na kuwadharau wanaume wasio kuwa na pesa kubadilika na mtazamo huo.


Zari aliandika ,“Pale unaposikia pesa za urithi hapo vipi?, mafanikio hayapatikani kupitia ngono mpenzi, endeleeni kudanga mkidhani kuwa wanaume matajiri watagonga kwenye miguu yenu na mafanikio yatapatika kwa usiku mmoja.“


“hata kama akifanya hivyo lakini atakuchukulia kama vitu vya samani kwamba atanunua vipya na kutupa vya zamani , kwangu mimi sio rahisi kunichukulia kirahisi, mimi ni msingi sio paa, hata hivyo tunaadhimisha mwaka mmoja wa kifo cha Ivan tangu afariki na ninafikiri ninahamasisha mtu popote alipo kupitia picha hizi za zamani “


“Usimdharau mwanaume asiyekuwa na kitu , Mungu ni wa wote, meza hugeuka , maskini! alifanya kazi usiku mchana kuninunulia hili gari akiwa na miaka 22 kwasababu aliona uanamke ndani yangu na hata nilivyojaribu hatukufanikiwa , tulianza kutokea chini si ndio , apumzike kwa Amani”

No comments

Powered by Blogger.