Full-Width Version (true/false)


Zari- Kuna Foleni Ya Wanaume Wanaonitaka Lakini Mimi Sipo Tayari

Mfanyabiashara maarufu na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady amefunguka na kudai kuna wanaume kibao wamepanga foleni wako tayari kuwa naye lakini yeye mwenyewe ndio hayuko tayari.

Zari alitokwa na povu hilo siku chache zilizopita baada ya kudaiwa amenunua gari lile ili amrushe roho Diamond na hata kudaiwa upweke alionao ndio unamsumbua na hata kudaiwa kuwa amekosa mwanaume wa kumhonga na kuwa naye.

Siku chache zilizopita Zari aliweka wazi kuwa amenunua gari jipya aina ya Range Rover Lakini mara tu baada ya hapo timu za Instagram zilimjia juu na kumsema kuwa ameazima tu gari lile ili amrushe roho Baba watoto wake na kudai hapo alipo ana upweke wa ajabu.

Zari alitumia mtandao wa Snapchat kuandika  ujumbe ambapo aliweka wazi kuwa hana upweke na wala hana shida ya  kuwa na mwanaume kwa sasa maana wapo wengi wanaomtaka:

".Oooh anajinunilisha magari kwa sababu hana raha, Hapana sio kweli Nipo Single kwa sababu nimeamua kuwa hivyo kwa sasa ..foleni ya wanaume wanaotaka kuwa na mimi ni kubwa sana lakini kwa sasa sitaki mtu... nikiwa tayari nitakuwa na Mahusiano lakini kwa sasa ni mimi na watoto wangu tu”.


No comments

Powered by Blogger.