Full-Width Version (true/false)


Zidane apata hofu Majeraha aliyoyapata Ronaldo

Meneja wa Mabingwa watetezi wa klabu bingwa Barani Ulaya timu ya Real Madrid, Zinedine Zidane ameonekana kupata hofu ya majeraha aliyopata mshambuliaji wake, Cristiano Ronaldo kwenye mchezo wa El Clasico uliyo pigwa hapo jana siku ya Jumapili na kumalizika kwa sare ya mabao 2 – 2.

Ronaldo ameonekana kupata majeraha ya kifundo cha mguu ‘ankle’ baada ya kuchezewa faulo na beki wa Barcelona, Gerard Pique hapo jana wakati akiipatia timu yake ya Madrid bao la kusawazisha dakika ya 15 ya kipindi cha kwanza.

Sio jambo zuri kwa muda huu lakini nafikiri kitakuwa nikitu kidogo, siwezi kusema atakuwa nje ya uwanja kwa muda gani ila kesho atafanyiwa vipimo vya ‘Scan’. Nadhani anafikiria kuwa siyo kubwa, hatuofii mchezo wa fainali ya klabu bingwa Barani Ulaya sote tutakuwepo.

Nyota huyo wa timu ya taifa ya Ureno mwenye umri wa miaka 33, ameonekana kuendelea na mchezo huo licha ya kutokuwa sawa hali iliyopelekea kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Marco Asensio mwanzoni mwa kipindi cha pili.

Kwa mara ya pili Real Madrid inatoka nyuma na kutoka sare ya 2 – 2 kwenye dimba la Camp Nou dhidi ya Barcelona ambayo haijapoteza hata mchezo mmoja kwenye ligi kuu ya Hispania Li Liga.

Madrid watawakabili Liverpool Mei 26 kwenye mchezo wa fainali wa michuano ya klabu bingwa Barani Ulaya huko Kiev huku, Zidane haamini kuwa Ronaldo kama amepata majeraha yatakayo muwezesha kutoshiriki mechi hiyo.

No comments

Powered by Blogger.