Full-Width Version (true/false)


Zimamoto yaokoa mabinti 100 Namthamini


 
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Juma Kwiyamba akizungumza mara baada ya kuwasilisha msaada huo kupitia kampeni ya namthamini.
 Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeunga mkono kampeni ya Namthamini inayoendeshwa kituo cha East Africa Televison (EATV) na East Africa Radio kwa kushirikiana na Msichana Initiative kwa kutoa mchango wa taulo za kike wenye thamani ya shilingi milioni 1.5.

Msaada huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam katika ofisi za EATV na Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Juma Kwiyamba kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa jeshi hilo Billy Mwakatage na kupokelewa na mkuu wa vipindi wa East Africa Radio Nasser Kingu.

Akiongea wakati wa utoaji wa taulo hizo za kike Kamishna Msaidizi Kuyamba amesema kuwa wameamua kutoa mchango huo kwa kutambua umuhimu wa mtoto wa kike kujistiri awapo kwenye siku zake ili aweze kuhudhuria shule na kufuatilia masomo kwa umakini.

“Jukumu letu sisi kama zimamoto ni kuokoa maisha na mali za watu hivyo kwa kufanya jambo hili tunaamini tumeweza kuwaokoa mabinti ambao East Africa LTD mliona tabu wanayoipata na mkaamua kuwathamini kwa kuanzisha hii kampeni hongereni sana”, amesema Kamishna Kwiyamba.


Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Juma Kwiyamba (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Vipindi wa East Africa Radio Nasser Kingu kifurushi chenye taulo za kike ambazo ni sehemu ya mchango wao waliowasilisha mapema asubuhi leo katika Ofisi za East Africa Televisheni LTD katika kufanikisha kampeni ya Namthamini.

Kwa upande wake Mwakilishi wa EATV aliyezunguka katika mikoa tofauti kugawa taulo za kike  kwa wanafunzi wa kike wa Sekondari, Belinda Semtandi, ameelezea namna msaada huo ulivyopokelewa kwa furaha na wanafunzi 2,265 walionufaika na msaada huo hadi sasa.

No comments

Powered by Blogger.