Full-Width Version (true/false)


Abdi Banda: " kucheza tena Bongo labda ipite miaka 10 "BEKI kiraka wa Baroka FC ya Afrika Kusini, Mtanzania, Abdi Banda, ame­funguka kuwa kwa sasa hana mawazo ya kurudi kucheza soka hapa nchini labda ipite miaka 10 ndiyo atarejea kujiunga na timu za hapa.

Ulipomalizika msimu wa 2016/17, Ban­da aliondoka ndani ya kikosi cha Simba na kutimkia Afrika Kusini ambako ameenda kucheza soka la kulipwa ndani ya kikosi cha Baroka alichosaini mkataba wa miaka mitatu na tayari amemali­za mwaka mmoja.


Beki huyo anayetumia mguu wa kushoto, ameliambia Gazeti letu Bora la Michezo la Cham­pioni Jumatatu, kuwa kwa sasa mawazo yake ni kuendelea kucheza soka la kulipwa zaidi na hata kama itatokea timu ya hapa Bongo ikimpa dau lolote, hatakuwa tayari kuja kujiunga nayo.


“Kwa sasa nawaza kwenda mbali zaidi ya hapa Afrika Kusini kwa ajili ya kujijengea zaidi juu ya maisha yangu ya soka, sitaki kuwa hapa Baroka ndiyo iwe mwisho wangu.


“Sina mawazo kabisa ya kurudi kucheza soka hapa Bongo kwa kipindi hiki, hata ikitokea timu ikanipa dau kubwa kiasi gani siwezi kuja kujiunga nayo labda ipite miaka 10 huko mbele kisha ndiyo nitakuja tena kucheza hapa,” alisema beki huyo wa zamani wa Coastal Union ya Tanga.

No comments

Powered by Blogger.