Full-Width Version (true/false)


Abdul Nondo alimsha dude kwa mara nyingine
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), wameuomba uongozi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya Bugando, kuwarudisha chuoni wanafunzi 10 waliofukuzwa na kusimamishwa chuo kutokana na sababu mbalimbali. 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumapili Juni 10, Mwenyekiti wa TSNP, Abdul Nondo, amesema  wanatarajia kuandika barua kwa kushirikiana na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), kwenda Wizara ya Elimu na TCU kupinga hatua zilizochukuliwa dhidi ya wanafunzi hao.

Tunaomba Wizara ya Elimu na TCU, kuratibu na kutofumbia macho vyuo vya aina hii ambavyo hujiamulia kwa matakwa yao wenyewe, hivyo vyuo vinapaswa kufuata taratibu na sheria zilizowekwa" Nondo.

Tunawaomba wadau wote wa elimu, viongozi wakiwamo wabunge, taasisi binafsi na Watanzania kwa ujumla kupinga kwa nguvu zote suala hili na kuomba kwa pamoja ili wanafunzi hao warudishwe chuoni kwani nchi bado inahitaji wasomi wakiwamo madaktari ambao nchi inawasomesha hivyo haiwezekani iwapoteze kwa mtindo wa aina hiyo".

Katika wanafunzi hao waliofukuzwa wamo viongozi wa Serikali ya Wanafunzi akiwepo aliyekuwa Rais wa Wanafunzi, Timoth Stephen, aliyekuwa Spika wa Bunge la Wanafunzi 2016/17, Godfrey Lameck na wengine nane waliosimamishwa kwa muda wa miezi tisa.

Wanafunzi hao wanadaiwa kupinga baadhi ya mambo hapo chuoni  ikiwamo kuondolewa kwa fedha za faini kwa wanafunzi waliochelewa kulipa ada na kupandisha ada bila kupitishwa na TCU na kukubaliwa na wanafunzi wenyewe.

No comments

Powered by Blogger.